Uswahiba wa Kim Jong Un na Trump ulivyowashangaza wengi

North Korean leader Kim Jong-un and US President Donald Trump meet in Hanoi, Vietnam. Photo: February 2019

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

Maelezo ya picha, Mkutano wa Hanoi wa mwezi Februari 2019 haukupangwa
Iliyochapishwa

Mkutano kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un utasalia kuwa tukio litakalokumbukwa kua muda mrefu kuhusu utawala wake.

Katika sehemu ya tatu na ya mwisho ya msururu wa makala ya BBC kuhusu utawala wa Trump ulivyochukuliwa duniani, tunaangazia maelezo mapya jinsi mkutano huo ulivyopangwa kwa kuzungumza na wale waliokuwa katika chumba wakati viongozi hao walipokutana

Kilichotokea kiliwashangaza hata wanadiplomasia mashuhuri - hasa tukio la Trump kubeba Kiongozi wa Korea kaskazini kwenye ndege yake rasmi ya Air Force One.

Mkutano wa pili kati ya Trump na Kim Jong-un, mjini HManoi, Vietnam, haukufanyika ulivyopangwa. Hii ni baada ya mashauriano kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini kuvunjika.

Trump aliondoka ghafla, na kuwaambia waandishi wa habari: "Wakati mwingine inabidi uende zako."

Lakini kabla ya kufanya hivyo, aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo alimpatia ofa ya kushangaza mwenzake Kim Jong Un wa Korea Kaskazini.

Matthew Pottinger, mtaalamu wa ngazi ya juu barani Asia kuhusu Baraza la Kitaifa la Usalama katika utawala wa Trump alituambia,: "Rais Trump alimpatia Kim lifti ya kwenda nyumbani Kim kwenye ndege yake aina ya Air Force One.

Rais alijua kwamba Kim alitumia treni uliyomchukua safari ya siku kadhaa kupitia China hadi Hanoi na hapo ndipo rais alimwambia: 'Naweza kukufikisha nyumbani ndani ya saa mbili ukiridhia ombi languc.' Kim alikataa."

Kosa ambalo 'sio la kulazimishwa'

Ofa ya kumpeleka Kim nyumbani, iliwaleta karibu viongozi hao wawili katika hatua ambayo haikutarajiwa. "Usuhuba" wao ulianzia Singapore, kwa mujibu wa Mshauri wa zamani wa Usalama wa Kimataifa John Bolton: "Trump alidhani amepata rafiki mpya."

Hapa, Trump alifanya kitendo kingine ambacho kiliwashangaza maafisa wake, wakati alipokubali ombi la Kim la kufutilia mbali zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini.

John Bolton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, John Bolton anasema kufutwa kwa zoezi la pamoja la kijeshi ni "hatua ambayo tulifikia bila kupata mbadala wake"

Bolton aliambia BBC: "Kim Jong-un, amekuwa akilalamikia zoezi kubwa la kijeshi kati ya Korea Kusini na vikosi vya Marekani, ambalo limekuwa likiendelea katika Rasi ya Korea kwa karibu miaka 60 au zaidi.

"Mara Trump, ghafla akasema, 'Nitafutilia mbali vita vya kitoto [kama alivyokuwa akiviitaa]. Hakuna haja ya kuwa navyo, ni ghafla mno na bila shaka utafurahia.' Sikuamini kusikia hilo.

" Mimi na [Waziri wa Mambo ya nje] Pompeo, [Mkuu wa wahudumu wa rais] Kelly tulikuwa ndani ya chumba cha mkutano na hatukushauriwa. Ni uamuzi wa kibinafsi wa Trump. Kosa ambalo sio la kulazimishwa; Tulikubaliana na ombi la Kim na hatukupata mbadala wake."

Maelezo zaidi:

2px presentational grey line

Ujumbe wa siri wa Trump kwa Kim

Kufanikiwa kwa mkutano huo kwenyewe kuliwashangaza wengi.

Miezi kadha kabla ya hapo, Trump alikuwa akimuita Kim "Jamaa wa Roketi" na kutishia Korea Kaskazini "fire and fury".Afisa wa ngazi ya juu katika Umoja wa Mataifa Jeff Feltman anaelezea jinsi, alivyowisilisha kisiri ujumbe wa Trump kwa Kim kuomba kukutana nae.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia masuala ya sias Feltman alikuwa amepewa mwaliko wa kwenda Pyongyang na Korea Kaskazini - lakini Wizara ya Mambo ya njebya Marekani ilitilia shaka mwaliko huo.

Hata hivyo, siku chache baadae, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alienda White House.

Feltman alituambia: "Walikuwa wanabadilishana mawazo kuhusu kile kinafanyika, huenda nini kikatokea, ni hatari kiasi gani, kuna uwezekano gani wa majeshi kuingilia miongoni mwa masuala mengine.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, alimwambia Rais Trump: 'Jeff Feltman amepewa mwaliko usiokuwa wa kawaida kwenda Pyongyang kuongoza majadiliano ya sera na Korea Kaskazini.'

"Nae Trump akamsongelea karibu na kumwambia: 'Jeff Feltman anastahili kwenda Pyongyang.Jeff Feltman anaweza kuiambia Korea Kaskazuni mimi niko tayari kukutana na Kim Jong-Un.''

Feltman alipuuzwa Pyongyang

Wakati Feltman alipozuru Pyongyang, aliisisitizia Korea Kaskazini uzito wa hali ilivyo:"Huo ndio ulikuwa ujumbe muhimu niliyojaribu kuwasilisha , kujibu hoja zao juu ya hitaji la kuzuia, ni kwamba kile wanachokiona kama kizuizi."

Maafisa wa UN waliomba kukutana faraghani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini kuwasilisha ujumbe wa kisiri kutoka kwa Trump.

Anakumbuka: "Kulikuwa na kimya kidogo kabla ya waziri wa mambo yanje kusema , 'sikuamini, kwa nini nikuamini.' Nami nikamjibu kwa kusema: 'Bwana fanya hivi, mimi siombi uniamini. Kile ninachokwambia ni kwamba UN ina ujumbe kutoka kwa Rais Trump; Mimi ndiye nilopewa ujumbe huo.'"

Alituambia: "Nilienda Pyongyang nikiwa mawazo mazito, ikizingatiwa hofu iliyokuwepo kwamba vita huenda vikatokea. Niliondoka Pyongyang nikiwa na uoga wa kujipata katika vita vya bahati mbaya ."

Trump alimwacha balozi wa Korea Kusini na mshangao

Kim hakujibu ujumbe wa Trump moja kwa moja - lakini miezi kadhaa baadae aliambia Korea Kusini kwamba yuko tayari kukutana na Rais wa Marekani.

Mshauri wa masuala ya usalama wa Korea Kusini alikimbilia White House kuwasilisha habari hizo.

Aliyekuwa Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Marekani wakati huo, HR McMaster, alielezea wakati Trump "aliporidhia" mkutano: "Balozi Chung hakuamini kilichofanyika kwani alidhani atakuwa na kibarua kigumu kushawishi ujumbe wake kukubalika."

Sawa na maafisa wengine wa White House, McMaster alikuwa na mashaka kuhusu mkutano wa Kim lakini, kama ilivyokuwa ada ya sera Trump ya mambo ya kigeni, rais angelikutana nae bila shaka.

Kama anavyosema McMaster: "Nilihisi ingelikuwa bora zaidi kama tungelimfanya Kim Jong-un asubiri jibu letu kwa muda kidogo. Lakini, rais hakuwa tayari kupoteza fursa hiyo."