Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Magufuli: Unaweza ukafa kwa malaria, unaweza ukafa kwa kansa, ukafa kwa magonjwa mengine
Rais wa Tanzaniwa John Pombe Magufuli amewataka Watanzania Wakristo na Waislamu kumuomba Mungu ili kuepuka ugonjwa ambao amesema mwaka jana ''Tuliushinda kwa kumtanguliza Mungu''. Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Katibu Mkuu kiongozi John Kijazi.
'' Ulipoingia ugonjwa huu wa kubana mafua mwaka jana tulimtanguliza Mungu pamoja na juhudi zingine mbalimbali, unapoona kitu huwezi kukitatua wewe muombe Mungu'', amesema Magufuli.
Marehemu Kijazi alifariki dunia baada ya kuugua na anatarajiwa kusafirishwa hadi Korogwe mkoani Tanga kwa mazishi siku ya Jumamosi.