Mkataba wa nyuklia wa Iran: Marekani iko wazi kwa pendekezo la mazungumzo 'wakati muhimu'

Rais Hassan Rouhani na mkuu wa teknolojia ya nyuklia Iran Ali Akbar Salehi wakikagua teknolojia ya nyuklia

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Marekani na nchi zenye uwezo barani ulaya zimetoa wito kwa Iran kurejelea utekelezaji wa nyuklia wa mwaka 2015.
Iliyochapishwa

Marekani imekubaliana na pendekezo la kushiriki katika mazungumzo yanayoihusisha Iran na nchi nyingine zenye ushawishi mkubwa duniani kwa lengo la kufufua mkataba wa nyuklia.

Iran iliapa kudhibiti mpango wake wa nyuklia kwa masharti ya kuondolewa vikwazo vya kiuchumi chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015.

Lakini rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa Marekani katika mkataba huo mwaka 2018, hatua iliyoifanya Iran kuvunja ahadi zake.

Sasa Marekani imeonesha nia ya kujiunga tena na mkataba huo chini ya utawala wa Rais Joe Biden.

Siku ya Alhamisi, Utawala wa Biden umekariri ahadi yake ya kujadiliana na Iran kuhusu mkataba huo, unaofahamika kama Mpango wa pamoja wa kina wa utendaji- (JCPOA).

Msemaji wa idara ya mambo ya nje Ned Price amesema Marekani itaitikia mwaliko wa Muungano wa Ulaya EU, katika mazungumzo ya Iran.

Eneo linalodaiwa kuwa na shughuli za mpango wa nyuklia wa Iran
Maelezo ya picha, Eneo linalodaiwa kuwa na shughuli za mpango wa nyuklia wa Iran

Mwanadiplomasia wa EU Enrique Mora aliandika katika Twitter yake kwamba yuko "tayari kualika" pande zote katika mazungumzo, akisema huu ni"wakati muhimu" kwa mkataba huo.

Iran haijatoa maelezo yoyote rasmi kuhusiana na pendekezo hilo.

Lakini katika ujumbe wa Twitter, Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif aliashiria kuwa nchi hiyo itazingatia mkataba huo kikamilifu endapo itaondolewa vikwazo iliyowekewa na Marekani.

Hali ya uhasama iliongezeka baina ya Iran chini ya utawala wa Rais Hassan Rouhani na utawala wa Marekani chini ya Rais Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hali ya uhasama iliongezeka baina ya Iran chini ya utawala wa Rais Hassan Rouhani na utawala wa Marekani chini ya Rais Trump

Iran imekuwa ikiishinikiza utawala wa Biden, kwa kutishia kuzuia ukaguzi wa kimataifa wa maeneo yake ya nyuklia ndani ya siku chache ikiwa Marekani haitaondoa vikwazo vyake.

Tangu Marekani ilipojiondoa katika mkataba huo, Iran, ambayo inasema mpango wake wa nyuklia ni salama, imerejelea au kuanza shughuli zake za nyuklia zilizokatazwa katika mkataba huo. Hatua hii imezua hofu miongoni mwa washirika ambao wanashuku nia ya Iran.

Wakijibu kwa pamoja, Marekani na washirika wake wa Ulaya- Uingereza, Ufaransa na Ujerumani- wametoa wito kwa Iran kutozuia ukaguzi, wakionya kwa pamoja kwamba hatua hiyo itakuwa "hatari".

Siku ya Alhamisi, nchi hizo nne zenye uwezo zilisema zitashirikiana kuhakikisha kwamba Iran "haitawahi kuuunda silaha za nyuklia".

2px presentational grey line

Mataifa ya Magharibi yaonya kuhusu hatua ya kurudi nyuma

Hii ni mara ya kwanza hatua kubwa ya kidplomasia kufikiwa kuhusu Iran zaidi ya miaka minne, mkutano wa awali ukitarajiwa kuongozwa na EU katika juhudi za kuondoa mkwamo unaozunguka suala hilo tata kuelekea utekelezaji kamili wa mkataba wa nyuklia.

Kama hatua ya kuonesha nia njema, utawala wa Biden umelegeza vikwazo vya usafiri dhidi ya wanadiplomasia wa Iran wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa vilivyowekwa na Bw. Trump. Pia ilibadilisha juhudi zake za kurejesha vikwazo vyote vya UN dhidi ya Iran.

Linapokuja suala la vikwazo vya Marekani, Bw. Biden anasema ataondoa mara baada ya Iran kuanza tena kuzingatia mkataba wa nyuklia.

Lakini Iran inataka vikwazo hivyo kuondolewa na Marekani kufikia wikendi hii, na kutishi akudhibiti ukaguzi wa mitambo yake ya nyuklia ikiwa haitafanya hivyo.

Mareakani na nchi za Ulaya zinapinga hatua hiyo wakiitaja kuwa inarudisha nyuma juhudi zilizofikiwa wakati wako tayari kuendelea mbele.

Iran inaonekana kana kwamba imepuuza tamko hilo lakini haijabainika ikiwa itaridhia mwaliko rasmi wa muzungumzo kuhusu suala hilo.

2px presentational grey line