Simulizi ya Kiran Dembla, mama wa nyumbani wa India aliyeamua kuujenga mwili

Iliyochapishwa

Wakati Kiran Dembla alipougua ugonjwa wa kuganda kwa damu kwenye ubongo wake, alikuwa anaishi maisha ya kawaida ya mwanamke wa nyumbani nchini India.

Alinusurika hatari hiyo ya kiafya, lakini matibabu aliyoyapata yalimfanya aongezeke uzito wa mwili. Kira aliamua kupambana na hali hii, na kubadili mtizamo wake kimaisha.

Sasa, akiwa mmoja wa wanawake wachache wa India waliojenga miili yao, anafanya kazi kama mkufunzi maarufu wa mafunzo ya mazoezi yanayoimarisha mwili akijivunia kuonesha pingili zake sita za mwili al maarufu six pack.