Meya wa Moshi:Nimewapiga marufuku kuvaa barakoa kwasababu wanaleta taharuki

Iliyochapishwa

Meya wa manispaa ya Moshi, Kaskazini mwa Tanzania Bwana Juma Raibu Juma amewataka wajumbe waliovaa barakoa katika kikao cha baraza la madiwani kuzivua kwa madai kuwa manispaa hiyo ipo salama.

Ametoa agizo hilo siku ya Alhamisi ,wakati wa ufunguzi wa kikao cha bajeti cha baraza hilo baada ya kuwataka waliovaa barakoa kusimama na kisha kuwataka wavue.

Aidha amesisitiza kuwa barakoa hizo huenda zikasababisha maambukizi kwasababu zinatoka mataifa ya nje.

Mwandishi wa BBC ,Scolar Kisanga ameongea naye na kumuuliza kwanini amechukua uamuzi huo;