Mamlaka ya mkoani Shinyanga yasema hakuna aliyeathirika na ulaji wa nguruwe
Iliyochapishwa
Tayari Serikali ya Wilaya ya kahama imepiga marufuku biashara na ulaji wa nguruwe katika eneo hilo ikilenga kutafuta kiini cha ugonjwa huo ambao umeua zaidi ya nguruwe 500 mpaka sasa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha amesema, mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitika kuathirika, lakini madhara ya homa hiyo, imefanya serikali ya wilaya yake, kuchukua hatua za haraka.
Amezungumza na mwandishi wetu Yusuph Mazimu na ameanza kwa kumueleza hatua iliyochukuliwa ni ya kisheria.