Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Uganda 2021: Bobi Wine asema Waganda wana fursa ya mwisho kuleta mabadiliko
Iliyochapishwa
Kampeini za uchaguzi mkuu nchini Uganda zinakamilika rasmi leo licha ya kuwa baadhi ya wagombea wa kiti cha urais tayari wamekamilisha mikutano yao ya kampeini.
Mgombea wa upinzani wa chama cha National Unity Party NUP Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amelalamika kuwa kampeini zake zimevurugwa kiasi kikubwa na utawala wa sasa.
Mwandishi wetu Roncliffe Odit alizungumza naye na kwanza anaanza kwa kumueleza jinsi kampeini zake zilivyokuwa.