Wangeci Waruire: Mwanamke Mkenya anayewalisha Wakenya waliopoteza kazi Dubai kutokana na corona
Iliyochapishwa
Mwanamke Mkenya amekuwa akipika chakula na kuwapatia Wakenya wenzake wanaoishi katika miliki za kiarabu UAE waliopoteza kazi kutokana na mlipuko wa corona.
Wangeci waruire alikuwa dereva wa teksi za Dubai wakati mlipuko wa corona ulipoanza.
Anasema kwamba alilazimika kujiuzulu kazi yake 2019 alipokuwa akipata mapato ya chini kukidhi mahitaji yake baada ya upande mmoja wa uwanja wa ndege kufungwa .
Mama huyo wa watoto watatu aligundua kwamba watu wengi hawana kazi ndiposa akaamua kuwapatia chakula cha bure.