Watu ishirini na watano wauawa huko DR Congo

Iliyochapishwa

Maafisa mashariki mwa Congo wamesema takriban watu ishirini na watano wameuawa katika mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na waasi wa kundi la ADF katika mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini mkesha wa mwaka mpya.

Mkuu wa wilaya ya Beni Donat Kibwana amesema raia hao waliuawa katika mashamba yao mkesha wa leo.

Awali Caro Robi amezungumza na mtetezi wa haki za binadamu huko Beni Eli Vahumawa kutaka kujua zaidi hali ikoje mjini humo.