Fahamu kwanini mwaka haumaliziki saa sita usiku wa Desemba 31?

Chanzo cha picha, Getty Images
Vifijo, nderemo na sherehe zisizo na kifani ni baadhi ya utamaduni kwa mamilioni ya watu kote duniani ambao hukusanyika kusherehekea saa sita usiku wa Desemba 31 ambapo mara nyingi watu huwa wamekusanyika na hata kuhesabu kadiri muda unavyokaribia kuingia mwaka mpya.
Kile watu wanachoamini wakati huo ni kwamba mwaka mmoja unaisha na mwaka mwingine unaingia, wakiwa na matumaini ya siku njema za baadaye hasa mwaka unaoingia na kujiwekea malengo chungu nzima, tayari kuyatimiza.
Ni siku ya mwisho katika Kalenda ya Gregori iliyoundwa kwa kuzunguka siku 365 pamoja na unaochukuliwa kuwa mwaka mrefu kama wa 2020.
Kalenda hiyo imekuwa ikitumika tangu kusitishwa kwa kalenda ya Yulio mwaka 1582.
"Kawaida huwa tunaelewa kuwa kuna mwaka, hasa kwa kuzingatia nyota na utamaduni mbalimbali kwa muda ambao sayari yetu huzunguka jua", amesema mtaalam wa masuala ya nyota Eduard Larrañaga, kutoka chuo kikuu cha Colombia.
Hata hivyo, kulingana na mtaalamu aliyezungumza na BBC Mundo, tarehe ambayo mwaka huanza na kumalizika hakuzingatii sayansi, ila ni dhana tu na kwamba huo ni mfumo endelevu.
"Kuchukulia kuwa mwaka unaisha saa sita usiku wa Desemba 31, na kuanza Januari 1, ni dhana tu tuliyojijengea," mtaalamu Larrañaga anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulingana na Larrañaga, kwa kuzingatia kwamba kufahamu kuwa mwaka umetimia kunatokana na muda unaotumika kwa dunia kuzunguka jua, kuhesabu ni lini hasa mzunguko huo unaanza na kumalizika, kiuhalisia kunaweza kutokea muda wowote ule.
"Kwa mtazamo wa mtaalamu wa nyota, hakuna kitu chochote kikubwa kinachotokea Desemba 31 ambacho unaweza kusema kuwa mwaka unaashia hapa, wala hakuna cha ajabu kinachotendeka unachoweza kusema Januari 1 ndio mwanzo wa mwaka, "anasema.
"Uhalisia wa mambo, katika kipindi chote cha mzunguko wa dunia hakuna kitu maalum au kisicho cha kawaida kinachotokea kuashiria kwamba mwaka umebadilika," anaongeza.
Lakini pia hili haliishi hapa.
Fikiria ya kwamba mwaka ni siku 365 au mwaka mrefu unaochukua siku 366, pia hiyo nayo ni dhana ambayo mwanadamu amejijengea tu mwenyewe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuhesabu mwaka kwa usahihi ni kitu kisichowezekana
Kulingana na wataalamu, ingawa wataalamu wa nyota wamejitahidi kuhesabu kwa usahihi kwa karne kadhaa muda unaochukua dunia kuzunguka jua lakini kumekuwa na tatizo ambalo linawazuia kupata siku sahihi za mzunguko.
"Pia urefu wa mwaka haufanani kabisa kwasababu kila kitu hubadilika kipindi cha mfumo wa jua na sayari zake.
Pia waweza kutazama:













