Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni vigumu kwa watu kuamini kuwa wanaume wanaweza kubakwa, lakini wameamua kujitokeza
Iliyochapishwa
Ubakaji wa wanaume ni jambo ambalo ni mwiko katika maeneo mengi ya dunia, ikiwa ni pamoja na Afrika ambako kuna unyanyapaa unaohusiana na jambo hilo. Watu wengi hudhani wanaume hawawezi kuwa wahanga wa ubakaji. Lakini waathiriwa wa ubakaji wanajitokeza barani Afrika, kuzungumzia juu ya uzoefu wao, kusaidiana, na kuhakikisha masaibu waliyopitia yanafahamika. BBC imezungumza na wanaume wawili mmoja kutoka Kenya na mwingine kutoka Tanzania. Taarifa hii imeandaliwa na kuhaririwa na Ashley Lime na Anne Okumu.