Isa Sulaiman, mwanaume wa Nigeria aliyeamua kumuoan mchumba wake licha ya wazazi kumkataa

SULAIMAN ISA/FACEBOOK

Chanzo cha picha, SULAIMAN ISA/FACEBOOK

Iliyochapishwa

Ni wapenzi waliozungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria hususan kutokana na utofauti wa umri, dini na asili zao na jinsi walivyofahamiana.

Isa Sulaiman mwenye umri wa miaka 26 anatarajia kufunga pingu za maisha na Mwanadada wa Kimarekani Janine Sanchez mwenye umri wa miaka 46.

Isa ambaye ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Maitama kilichopo katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria anatarajia kumuoa mchumba wake Janine ambaye ni mpishi katika Mgahawa wa Afghanstan uliopo California Jumapili hii.

Wapenzi hao walizua gumzo kubwa mtandaoni hususan pale Janine alipotembelea nchini Nigeria miezi kadhaa baada ya kuwasiliana na mpenzi wake kwa njia ya jumbe na video mtandaoni.

Wakazi wa kano waliwazungumzia na kuwafuatilia maisha yao tangu alipowasili katika jimbo hilo na Isa anasema alishindwa hata kumtembeza mpenzi wake katika maeneo kama sokoni na madukani kutokana na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiwashangaa kila mara walipowaona wakitembea barabarani pamoja.

Janine na Isa Sulaiman walifahamiana kwa njia ya mtandao na kuamua kuoana
Maelezo ya picha, Janine na Isa Sulaiman walifahamiana kwa njia ya mtandao na kuamua kuoana

Ndoa yao ilikuwa imepangwa kufanyika mwezi Machi lakini iliaahirishwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Lakini baada ya miezi kadhaa ya subra , hatimaye ndoa yapo itafanyika na sasa familia ya Isa imeamua kuwaunga mkono na kuipa baraka ndoa yao licha ya kwamba mwanzoni walikuwa wamekataa kutokana na hofu ya kwamba mtoto wao hafahamiani na mchumba wake waliyekutana kwa mara ya kwanza kwa njia ya mtandao.

baba yake Isa Mzee Mallam Isa Panshekara ambaye ni polisi mstaafu amesema hakuna kitu kinachoweza kuwa sawa kwa asilimia 100, kwa hiyo ameamua kuwapa baraka na ameahidi kuwaombea baraka.

" Kama mtu ninayefahamu masuala ya usalama nilihakikisha wakati wa harusi kunakuwa na usalama wa kutosha na tayari nimetembelea kamati ya Sharia kuongea na viongozi wa kidini , kwa hiyo hakuna tatizo ."

Kuhusu harusi yao , wapenzi hao wameshauriwa wasifanye sherehe zozote za harusi, isipokuwa sala ya ndoa itakayofanyika katika msikiti Jumapili kutokana na hofu ya usalama wao.

Jimbo la Kano nchini Nigeria limekuwa likikabiliwa na mashambulio ya Waislam wenye itikadi kali.

Mallam Isa Panshekara afisa wa zamnai wa polisi alisema alisema hawanabudi kwa hiyo wameamua kuibariki ndoa ya mtoto wao.

Chanzo cha picha, SULAIMAN ISA/FACEBOOK

Maelezo ya picha, Mallam Isa Panshekara afisa wa zamnai wa polisi alisema alisema hawanabudi kwa hiyo wameamua kuibariki ndoa ya mtoto wao.

Mallam Isa Panshekara afisa wa zamnai wa polisi alisema alisema hawanabudi kwa hiyo wameamua kuibariki ndoa ya mtoto wao.

"Kwa hiyo kando na sala ya harusi msikini hakuna kitu kingine kama sherehe kitakachofanyika kutokana pia na hali iliyopo nchinimwetu na pia jinsi gharama ya maisha ilivyopanda wakati huu, kukodisha ukumbi wa sherehe ni pesa nyingi . Lakini tutakapokwenda Marekani tutafanya sherehe kubwa huko .", alisema Isa.

"Kuhusu sala ya harusi, Janine alitaka kuhudhuria lakini tukamwambia kuwa wanawake huwa hawashiriki sibala ya ndoa msikitini pamoja na wanaume ."

Tunamkosa mtoto wetu atakapohamia Marekani na mke wake ,Baba yake Mallam Isa alisema.

Aina hii ya ndoa ambapo mke anamzidi umri mwanaume na pia kwa wao kufahamiana kwa njia ya mtandao sio ya jambo la kawaida nchini Nigeria na ndio maana watu wengi wamekuwa wakiifuatilia kufahamu hadi mwisho wake

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti, Marehemu wanaofunga ndoa Tanzania