Nigeria kitovu cha utapeli wa kimtandao

Maelezo ya video, Nigeria kitovu cha utapeli wa kimtandao
Iliyochapishwa

Barua pepe za kibiashara ni moja ya uvamizi wa kimtandao unaofanyika sana duniani huku shirika la Ujasusi la Marekani likisema utapeli huo unagharimu karibu dola bilioni 9 kwa mwaka na wataalamu wanasema Nigeria ndio kitovu cha uvamizi huo.

BBC imezungumza na mmoja wa wavamizi kujua namna wanavyofanya kazi zao na vile anavyohisi kuhusu waathirika.