Familia ya Mberesero imesema haijapokea taarifa rasmi kuhusu kifo cha kijana wao

Maelezo ya sauti, Familia ya Mberesero yasema haina taarifa rasmi kuhusu kifo cha kijana wao
Iliyochapishwa

Familia ya mtanzania anayedaiwa kujinyonga gerezani nchini, imesema mpaka sasa haijapata taarifa rasmi ya kifo cha kijana wao huyo, aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika shambulio la kigaidi la mwaka 2015 nchini Kenya.

Shambulio hilo lililofanywa katika chuo kikuu cha garisa lilisababisha vifo vya watu 148.

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba, Rashid Charles Mberesero, aliyekamatwa mwaka jana na wenzake wawili, alijinyonga kwa kutumia blanketi, kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti.

Baba wa kijana huyo amezungumza na Scolar Kisanga.