Mzozo wa Ethiopia: Watu wawili wapoteza maisha kutokana na shambulio la anga Tigray

Maelezo ya video, Mzozo wa Ethiopia: Athari za shambulio la anga mjini Mekelle, Tigray
Iliyochapishwa

Shambulio la anga kabla ya mchana siku ya Jumanne liliua watu wawili na kujeruhi wengine huko Mekelle. Madaktari wameeleza.

Haijulikani bado ni nani alitekeleza shambulio hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limesema maelfu ya watu wamekimbia mapigano.