Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Je ushindi wa Biden una maana gani kwa Iran, Israel, Korea kaskazini china na Urusi?

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya siku kadhaa za hali ya wasiwasi , Joe Biden ameshinda uchaguzi wa Marekani.
Wakati wa kipindi cha miaka minne iliopita , uhusiano wa Marekani na ulimwengu ulibadilika ghafla. Wanahabari wa BBC duniani , kutoka Beijing hadi Berlin , wanaelezea jinsi habari za ushindi wa Joe Biden zilivyopokelewa na maana yake kwa mahusiano muhimu ya Marekani.

Joe Biden anatoa changamoto mpya kwa serikali ya China aliandika mwandishi John Sudworth mjini Beijing.
Unaweza kufikiria kwamba Beijing ingelifurahia sana iwapo Donald Trump angeshindwa. Alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele kuikashifu China mara kwa mara na kuiwekea vikwazo kadhaa mbali na kuilaumu kwa virusi vya corona.
Lakini wachambuzi wanasema kwamba uongozi wa China huenda sasa unahisi kutofurahishwa na kushindwa kwake , Sio kwasababu wanampenda bali kwasababu alikuwa anaiharibu Marekani kwa kuwa mgawanyaji nyumbani na kuharibu uhusiano wake na mataifa mengine.
China ilidhani kwamba muhula mwengine wa Trump ungeliporomosha uchumi wa Marekani na kusababisha kuanguka kwa uwezo wake.

Mizizi ya Kamala Harris ni chanzo cha majivuno kwa India ;lakini Narendra Modi huenda akawa na uhusiano usio mzuri na Joe Biden ikilinganishwa na mtangulizi wake anasema. Rajini vaidnathan kutoka Delhi.
India imekuwa mshirika mkubwa wa Marekani na kwamba uhusiano huo hautabadilika chini ya Uongozi wa Biden
Hatahivyo uhusiano kati ya viongozi hao wawili huenda ukachukua mweleko usio wa kawaida. Bwana Trump amekuwa akizuia kuzikosoa sera zenye utata za Modi ambazo wengi wanasema zimekuwa zikiwabagua Waislamu. Lakini bwana Biden amekuwa wazi , Tovuti yake ya kampeni imekuwa ikitaka haki kupatiwa raia wa Kashmir .

Korea kaskazini ambayo kuna wakati ilimuita Joe Biden 'mbwa koko', lakini sasa Kim jong un atalazimika kufanya hesabu zake vizuri kabla ya kumchokoza rais huyo mpya kulingana na mwandishi Laura Bicker mjini Seoul.
Ni wazi kwamba Kim angependelea tena muhula mwengine wa miaka minne ya rais Donald Trump.
Mikutano ya viongozi hao wawili ilileta picha za kihistoria lakini hakuna kikuu kilichoafikiwa. Hakuna hata pande moja iliopata kile ilichokuwa ikitarajia.
Korea Kaskazini imeendelea kujenga silaha za kinyuklia na Marekani imeendelea kuiwekea vikwazo. Badala yake Joe Biden ametaka Korea kaskazini kuonyesha kwamba ipo tayari kuwacha utengenezaji wa silaha za kinyuklia kabla ya kufanya mikutano yoyote na Kim Jong un.
Wachambuzi wanasema kwamba iwapo rais Biden hatoanzisha mazungumzo ya haraka na kiongozi huyo huenda hali ya chuki kati ya mataifa hayo mawili ikarejea. Kim jong un huenda akataka kuilazimisha Marekani kurudi katika meza ya mazungumzo kupitia majaribio ya makombora yake.

Moscow inahofia kwamba Biden ataiwekea shinikizo na vikwazo zaidi . Huku mgombea wa Democrat akiingia Ikulu ya Whitehouse je ni wakati wa kulipa kisasi cha Urusi kuingilia uchaguzi wa 2016?
Moscow fears the Biden presidency will mean more pressure, more sanctions from Washington.

Ushindi wa Biden unaweza kuirudisha Iran katika meza ya majadiliano anaandika mwandishi wa BBC Persia Kasra Naji.
Wiki chache kabla ya uchaguzi wa Marekani , rais Trump alisema kwamba atakapochaguliwa kwa muhula wa pili simu ya kwanza atakayopokea itakuwa kutoka kwa Iran ikitaka waanze mazungumzo mapya kuhusu mipango yake ya kinyuklia.
Hatahivyo mazungumzo yoyote na rais Trump yasingefanyika . Chini ya uongozi wa Trump vikwazo vya Marekani vimeiwacha Iran kukaribia kuanguka kiuchumi.
Pia aliagiza kuuawa kwa jenerali Qasem Soleimani rafiki wa karibu wa kiongozi wa kidini wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.
Negotiating with a Trump administration would have been impossible; it would be too humiliating.

Kuna matumaini ya mabadiliko ya kisera za rais Donald Trump katika eneo la mashariki ya kati. Anaandika mwndishi Tom Bateman mjini Jerusalem.
Rais Trump aliwapendelea sana washirika wake katika eneo hilo huku akiitosa Iran.
Rais Mteule Biden atajaribu kurudisha sera za Marekani katika eneo hilo ilivyokuwa wakati akiwa makamu wa rais wa Marekani chini ya rais Obama.
Akipunguza shinikizo kali dhidi ya Iran na kurudisha makubaliano ya amani ya nyuklia yaliofutiliwa mbali na Trump miaka miwili iliopita.
Hali hiyo itaikasirisha Israel na mataifa ya mashariki ya kati kama vile Saudia na UAE.
Waziri mmoja wa Israel alisema akijibu ushindi wa Biden kwamba sera hiyo itaisha na vita kati ya Israel na Iran kwasababu 'tutalazimika kuchukua hatua'.












