Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Mbunge wa upinzani aliyeshinda uchaguzi
Iliyochapishwa
Matokeo ya uchaguzi mkuu Tanzania bado yanaendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini humo. Kwa mujibu wa Tume hiyo asilimia 60 ya matokeo ya urais yameshatangazwa huku katika majimbo zaidi ya 150 yaliyotufikia baada ya kutangazwa na tume, ni majimbo mawili tu yamechukuliwa na upinzani mpaka sasa, huku majimbo yaliyotazamwa kama ngome ya upinzani kwa miaka mingi, yakinyakuliwa na chama tawala, cha CCM.
Mbunge mmojawapo wa upinzani aliyetangazwa kushinda ni Shemsia Mtamba, wa Mtwara vijijini aliyemshinda Hawa Ghasia, mmoja wa vigogo na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya Taznania kwa vipindi tofauti. Tumemuuliza kwanza amejisikiaje kupata ushindi huo?
