Uchaguzi wa Marekani 2020: Jinsi Kamala Harris anavyoangazia kinachowakabili wanasiasa wanawake

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati Seneta Kamala Harris alipoandikisha historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mgombea mweza wa urais katika uchaguzi wa Marekani, bila shaka ilikuwa vigumu kujiepusha na suala la jinsia kipindi hiki cha uchaguzi- Lakini Je wanawake katika siasa wanachukuliwa tofauti?
Hivi ndivyo uteuzi wake unaangazia maswala ambayo wanawake katika siasa wamekutana nayo kwa miongo kadhaa - na jinsi mabo yanavyo badiliaka - katika uchambuzi huu kutoka kwa Debbie Walsh, Mkurugenzi wa Kituo cha Wanawake na Siasa za Amerika katika Chuo Kikuu cha Rutgers.
Sanaa ya kutokuwa na hasira
Wanawake wanapoingia kwenye siasa wanatakiwa kujiamini na kuthubutu.
Wanatakiwa kutumia busara zote kujiwasilisha kwa watu bila kupoteza muelekeo wao.
Utafiti unaonesha kuwa ubaguzi wa kijinsia ambao umekuwepo tangu jadi huenda ukawafanya wanasiasa wanawke kueleweka visivyo katika masuala ambayo kwa mfano wenzao wa kiume wanaweza kusifiwa kama ishara ya ukakamavu.
Kwa wanawake wanaotokea jamii ya wachachu, ubaguzi huo wa kijinsia pia unakabiliwa na changamoto ya ubafuzi wa rangi. Nchini Marekani misemo kama "mwanamke mweusi mwenye hasira" yametumika kibaguzi kwa muda mrefu. Msemo huo uliibuka karne ya 19, kuwaangazi awanawake weusi kama watu wasiokuwa na ustaarabu na wasio na mantiki.
Kama anavyoelezea Bi Walsh: "Wanawake wamelaumiwa kwa kutokuwa na uwezo na nguvu ya kuwa rais au makamu wa rais, lakini wakati huo huo, unaonyeshaje nguvu bila kuonekana kama mtu mwenye hasira?"
Anahisi Bi Harris alifanya kazi nzuri kufuata nyayo katika mjadala wa makamu wa rais, lakini anaongeza kuwa wakati mwingine alionekana kana kwamba anajizuia kusema kila kitu - japo majibu yake ya upole alipokatizwa kuzungumza na mwenzake yalikuwa ''mazuri'' kwa mwanamke yeyote aliye na uzoefu wa kukabiliana na hali kama hizo.
Je anatosha kuongoza?
Baadhi ya wachambuzi wanasema wanawake wanapaswa kujithibitisha kwenye kampeni kwa njia ambazo wanaume hawafanyi, hata kama jinsia haliwatii hofu wapiga kura. Pale ambapo watu wanachukulia uwezo kwa wanaume ni jambo la kawaida, wanawake lazima waonyeshe.
Kura ya maoni iliyofanywa na Economist/YouGov mwezi Agosti ulionyesha kuwa makamu wa rais aliyepo madarakani aliongoza kwa uchache wa kura za watu wanaompendelea akilinganishwa na bI Harris. Robo ya Wamarekani walioshirika kura hiyo ya maoni hawakuwa na uhakika kuhusu uongozi wa Bi Harris, huku asilimia 14 wakitoa kauli sawana hiyo kumhusu Bw. Pence.
Baada ya mjadala huo baadhi ya wapigakura walihisi Harris alishinda. Lakini walipoulizwa ni nani bora kuchukia nafasi ya rais baadhi yao walionekana kuwa na mtazamo tofauti.
Kura ya maoni ya YouGov, ilibaini kuwa Wamarekani wengi - asilimia 56 - walihisi Bw. Pence alikuwa na nafasi nzuri kuwa rais ikiwa Bw. Trump hataweza kuhudumu, huku asilimia 50 ya wengine wakiwa na maoni sawia na hayo kumhusu Bi Harris.
Japo baadhi ya walioshiriki kura hiyo ya maoni huenda wakafikiria makamu wa rais aliye madarakani amehitimu zaidi kwa nafasi hiyo ya juu akilinganishwa na seneta wa mara ya kwanza, wanaharakati wanaotetea haki ya wanawake katika siasa kwa muda mrefu wameonesha uwezo wao zaidi ya wenzao wa kiume.
Kuwa 'Momala'
Alipokubali nafasi ya kuwa mgombea mwenza katika chama cha Democratic, Bi Harris alisema wadhifa wa makamu wa rais utakuwa mzuri sana, "lakini 'momala' ina maana zaidi ".
Alipojitambulisha kwa Wamarekani, Bi Harris mara nyingi aliangazia familia yake ( yeye ni mama wa kambo wa watoto wawili) na maadili yao. Namna alilelewa na mama mmoja pamoja na familia yake mchanganyiko imekuwa muhimu kwa jinsi Bi Harris anavyojinadi kama mgombea mwenza.
Kwa wanaume katika siasa, Bi Walsh anasema, kutambulisha familia zao "daima imekuwa kuongeza thamani". Lakini ni hivi majuzi tu ambapo wanawake katika siasa pia wameanza kutumia uzoefu wao kama sifa.
Ni hali "ngumu kwa wanawake", anasema, kwasababu ikiwa hawana watoto wala kuwazungumzia maswali yanaibuliwa "kwanini?" "Halafu wakiwazungumzia hasa wakiwa wadogo unaulizwa ni nani atawatunza watoto wako linaibuka?"
Hali ni tofauti kwa wanaume, wakati mwanamume anapozungumzia familia yake, anajenga taswira ya kuwa "kiongozi wa familia", lakini "hakuna mtu yeyote anayemuuliza jinsi anavyowajibikia familia [yake]", au hata kuuliza ni nani atawatunza watoto.
Mfano mzuri wa kufafanua hali hii ni kupitia Sarah Palin ambaye mjadala kuhusu familia yake ilizua gumzo alipoteuliwa kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi wa 2008.
Bi Palin ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Alaska alijipata akielezewa darubini na vyombo vya habari na wafuasi wa Democratic waliotaka kubaini jinsi alivyo wajimbikia familia yake.
Wakati huo Bi Palin alikuwa na watoto watano na mmoja alikuwa na ulemavu. Wakosoaji wake waliuliza ikiwa atatelekeza familia yake kugombea nafasi ya juu ya uongozi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini hali hiyo ya ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanasiasa wa kike imeanza kubadilika - japo inakuwa vigumu kwa wanawake katika siasa kuepuka swali uzazi.
Bi Walshpia anaongeza kuwa Kamala Harris yuko katika nafasi ya kipekee kama mama kwa watoto wa kambo ambao sasa ni watu wazima.
Na ki uhalisia, wapiga kura wanataka kuwaona wagombea wao kama wanadamu wa kawaida waliyo na maisha yao binafsi.
"Kwa hivyo nadhani anafanya jambo ambalo la kiuhalisia"

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaume walisema nini kumhusu?
Donald Trump amemkumbuka vizuri sana, usiku wa Jumanne alisema, "Harris alikuwa mbaya kwa mtu wa pili alieteuliwa katika Mahakama ya juu zaidi aliymuonesha maudhi, Brett Kavanaugh.
Bw. Trump aliongeza kuwa ni mtu mwenye misimamo mikali na asiye na heshima n mwenye chuki: Hayo ndio maneno aliyotumia kumuelezea Harris alipokuwa mgombea mwenza wa Joe Biden.
Mpinzani wake Mike Pence hakutumia maneno ya matusi dhidi yake, lakini alimrushia madongo wakati wa mdahalo wa makamu wa rais .
Kamala Harris alipoanzisha kampeni yake mbele ya maelfu ya wafuasi wake Januari 2019, alichukuliwa kama mgombea wa juu. Wakati fulani, Julai, baada ya mdahalo wa kwanza aliokuwa amebobea, aliongeza ushawishi wake katika kura za maoni za awali.
Harris amepitia changamoto zake na anajua mtu anaweza kukumbana na yapi. Kama angekuwa mtu dhaifu, tayari angekuwa ameshafahamika kufikia sasa lakini almuradi ameamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombea kiti cha juu zaidi, inawezekana siku moja Wamarekani wakaanza kumfikiria kama rais.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mambo yamebadilika vipi?
Bi Walsh anasema mwaka 2018, ulishuhudia ongezeko kubwa la wanawake waliojitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania nyadhifa za kisiasa'
"Wanawake hawakutumia muda mwingi kufukiria 'natakiwa kufanya nini' bali walijinadi wao kama wao," anasema. "Tulishuhudia hilo mwaka 2018 wakati wagombea wengi walikuwa wakizungumzia masuala ambayo wanawake wameshauriwa kujitenga nayo."
Masuala hayo ni kama kutotaja watoto wao, kuangazia changamoto yao maishania u kuzungumzia matatizo ya kifedha yanayowakabili.
Mwaka 2017, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice pia alitoa wito kwa wanawake kutokubali "mtu yeyote kuwabagua kwa misingi ya kijinsia au rangi ya ngizi yao".
"Hiayo ni mambo lazima tuwaambie wanawake: Unapoingia katika chumba cha mkutano, ikiwa mtu atajaribu kukudunisha, usikabiliane naye. Unachotakiwa kufanya nikujieleza kwa utulivu bila hasira," alisema lkatika kongamano la uongozi la KPMG.
"Ikiwa unahisi huenda umezuiliwa kitu ambacho unadhani ulistahili kupata, kuna njia nyingi ya kukitafuta - na una haki ya kihakikisha unakipigania hadi ukipate."
Bi Walsh anasema kuanzia Geraldine Ferraro hadi kwa Sarah Palin na Hillary Clinton, kila mgombea amejiimarisha kutokana na tajiriba aliyopata zamani. Na sasa tumefikia kiwango ambacho mwanamke mweusi mwenye asili ya kihindi ameteuliwa kuwa mgombea mwenza wa urais ", alisema.
"Wakati wanawake wanapomuona mtu kama Kamala Harris akiteuliwa kama mgambea mwenza wa rais wanamchagua wakiwa na matumaini huenda akawa makamu wa rais, hatua hiyo tu inabadilisha mtazamo wa kile wanaweza kuwa maishani "












