Uchaguzi Tanzania 2020: Changamoto za wasiosikia wakati wa kampeni
Iliyochapishwa
Wakati Kampeni zikielekea ukingoni nchini Tanzania watu wasio sikia (Viziwi) wanasema wanaomba jitihada zaidi kufanyika na Tume na vyama vya siasa ili nao waweze kuchagua viongozi wao kutokana na sera zao badala ya kutazama sura.
Mwandishi wa BBC Eagan Salla akiwa Jijini Mwanza alikutana na Jones George na Salome Sospeter ambao walihudhuria Kampeni kwa Mara ya kwanza.