Uchaguzi Tanzania 2020: Katibu mkuu wa CCM Tanzania Bashiru Ally azungumzia vipaumbele vya chama

Maelezo ya sauti, Bashiru Ally: Uhuru ni kama njaa ukila unahitaji kula zaidi
Iliyochapishwa

Kampeni nchini Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ziko dakika ya lala salama, kila mgombea awe wa ubunge, udiwani na wa Urais wanafanya juu chini kunadi sera zao.

Kwa wale ambao hawajashika dola wakijaribu kushawishi wapiga kura mambo wanayotarajia kufanya huku chama tawala kikijiuza kwa mambo ambayo kimefanya na pia matarajio yao.

Katika kutaka kujua malengo yao na kuwajua wagombea kwa undani tumekuwa tukizungumza na baadhi yao, Hata hivyo kwa Chama tawala cha CCM hatukufanikiwa kumpata mgombea na badala yake tumefanya mazungumzo na Katibu mkuu wa chama hicho Bashiru Ally, mwenzetu Zuhura Yunus alizungumza nae na kumuuliza vipaumbele vyao ni nini.