Je mwanafunzi mjamzito ni sahihi kurejea shuleni katikati ya janga la corona?

Iliyochapishwa

Shule za msingi na za sekondari zimefunguliwa rasmi nchini Kenya, baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi 6 kutokana na janga la Corona.

Wazazi wengi wamekuwa wakilalamikia kutokuwa na karo ya shule.

Waziri wa elimu nchini Kenya Prof George Magoha amesema wazazi wasiwe na sababu kwa watoto kukosa kwenda shule na hata wanafunzi waliopata uja uzito pia nao waripoti shuleni kuendelea na masomo yao.