Je ni kwanini rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini alikuwa na hasira wakati wa hotuba hii?

Iliyochapishwa

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alijawa na hisia chungu nzima wakati wa hotuba katika hafla ya gwaride la kijeshi wikendi iliopita.

Alifuta machozi wakati alipokuwa akizungumza kuhusu changamoto linalopitia taifa hilo.

Huku jeshi la taifa hilo likionesha silaha mpya , Kim Jong un aliwashukuru wanajeshi wake kwa juhudi zao dhidi ya mlipuko wa corona na majanga ya hivi lkaribuni.

Wachunguzi wanasema kwamba huenda anajaribu kuonesha unyenyekevu wakati ambapo taifa hilo linakabiliwa na mzozo wa kiuchumi