Tuzo ya Nobel 2020: Shirika la Chakula Duniani WFP ndio mshindi wa tuzo hiyo ya amani

Shirika la Chakula Duniani WFP linasema kwamba lilitoa usaidizi kwa takriban watu milioni 100 mwaka uliopita

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2020 imezawadiwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Chakula Duniani World Food Programme .

Kamati ya tuzo hiyo nchini Norway ilisema kwamba WFP ilihusika pakubwa katika juhudi za kuzuia utumiaji wa njaa kama silaha ya vita na mizozo.

Tuzo hiyo ina thamani ya $1m. Mshindi wa 101 wa tuzo hiyo alitangazwa katika taasisi ya tuzo hiyo mjini Oslo.

Msemaji wa WFP amesema kwamba anajivunia tuzo hiyo. Shirika la Chakula Duniani linakadiria kwamba huwasaidia watu milioni 97 kila mwaka katika mataifa 88.

Msemaji wa WFP amesema kwamba anajivunia tuzo hiyo.

Ni nini ilichosema kamati ya Tuzo hiyo?

Shirika la chakula duniani linakadiria kwamba huwasaidia watu milioni 97 kila mwaka katika mataifa 88.

''Kutokana na tuzo ya mwaka huu, kamati hii inataka dunia kuangazia kuhusu mamilioni ya watu ambao wanakabiliwa na tishio la baa la njaa'', alisema Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo mjini Oslo Berit Reiss - Andersen.

Berit Reiss-Andersen alimtangaza mshindi wa tuzo hiyo mjini Oslo

Chanzo cha picha, EPA

Shirika la Chakula Duniani lina jukumu muhimu katika ushirikiano wa kimataifa ili kuhakikisha kuwa chakula kinatumiwa kuleta amani.

Takriban wa 211 ikiwemo mashirika 107 waliteuliwa kuwania tuzo hiyo mwaka huu.

Chini ya sheria za wakfu wa tuzo hiyo walioteuliwa katika orodha ya kuwania tuzo hiyo hawafai kuchapishwa kwa miaka 50 na shirika hilo linasema kwamba uvumi wowote kabla ya tangazo la mshindi wake unafaa kuchukuliwa kama uvumi.

Shirika la Afya Duniani na mwanaharakati wa masuala ya anga Greta Thunberg walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakipigiwa upatu kushinda tuzo hiyo.

Je ni akina nani walioshinda tuzo hiyo siku za nyuma?

Tuzo ya amani ya Nobel mwaka uliopita ilichukuliwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed , ambaye makubaliano yake ya amani na Eritrea yalisitisha uhasama kufuatia vita vyao vya mpakani vya 1998-2000.

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama alishinda tuzo hiyo mwaka 2009 katika juhudi zake za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano kati ya raia.

Wengine walioshinda ni pamoja na rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter {2002}, Mwanaharakati wa elimu ya watoto Malala Yousafzai, Shirika la Umoja wa mataifa na katibu wake wakati wa Kffi Annan{2001} na mama Teresa {1979}.