Waumini wa Kikristo wanasema nini kuhusu uchaguzi wa Marekani
Iliyochapishwa
Yamebaki majuma machache kabla ya uchaguzi wa urais muhimu zaidi wa Marekani kuwahi kutokea. Wagombea wote wameweka dini katikati ya kampeni zao.
Ingawa wainjilisti weupe walimsaidia Donald Trump kuingia Ikulu mnamo 2016, mwaka huu suala hilo ni ngumu zaidi.
Katika jimbo la North Carolina kuna kiwango cha chini ya asilimia kati ya wagombea wawili. Kwa hivyo wapiga kura Wakristo wanasema nini?