Msajili wa vyama Tanzania: Miungano ya vyama inapaswa kuwasilishwa kwa msajili wa vyama miezi 3 kabla uchaguzi

Iliyochapishwa

Afisi inayosimamia usajili wa vyama nchini Tanzania imesisitiza kuwa vyama vya kisiasa vinapaswa kuheshimu sheria vinapoingia katika ushirikiano wa aina yoyote ama miungano kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.

Afisi hiyo imesema kwamba vyama hivyo vinapaswa kuwasilisha ushirikiano au muungano huo kwa msajili wa vyama miezi mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.