Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchunguzi wa BBC watofautiana na madai ya chanzo cha ajali ya Moto katika shule ya Nigeria
Iliyochapishwa
Ushahidi mpya ambao kipindi cha BBC Africa Eye kimeupata ni kinyume na maelezo rasmi kwamba mlipuko wa moto , uliowauwa watu 23 na kuharibu shule ya malazi ya wasichana nchini Nigeria, ilikuwa ni ajali iliyotarajiwa. Kampuni ya mafuta ya ya kitaifa ya Nigeria, inayomilikiwa na taifa, ilidai kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya lori kugonga bomba la gesi lililopo karibu na mabomba ya petrol. Lakini ushahidi mpya unaonesha kuwa maelezo haya kuhusu chanzo cha mlipuko ulioenea kwenye eneo la kilomita za mraba 100,000 za mji wa Lagos, sio sahihi.