Mafanikio na changamoto ya 'Elimu bila ada Tanzania'

Maelezo ya video, Mafanikio na Changamoto ya 'Elimu Bila ada Tanzania'
Iliyochapishwa

Serikali ya Tanzania chini ya rais John Magufuli  ilipitisha waraka wa  Elimu Namba 6 wa Mwaka 2015 kuhusu utekelezaji wa elimu bure kwa shule  sekondari.

Waraka huo ulioanza kutekelezwa Januari 2016  umechangia kuinua sekta ya elimu na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza licha ya changamoto kadhaa  kujitokeza.

Awali elimu ya msingi ilikuwa ni bure huku shule za secondari ilipiwa ada kiasi cha dolla 17.