Ngiri maji yenye uzito wa kilo 20 yavunja ndoto ya mkulima Tanzania

Maelezo ya video, Ngiri maji yenye uzito wa kilo 20 yavunja ndoto ya mkulima Tanzania
Iliyochapishwa

Hujafa hujaumbika. Ni maneno ya wahenga. Hii inaonekana dhahiri katika maisha ya kijana Matayo Kudenya, mkazi wa kizota, jijini Dodoma.

Kudenya ambae awali alikuwa akijishughulisha na ukulima, kwa miaka kadhaa sasa shughuli zake zote zimesimama kutokana na tatizo la ngiri maji au busha ambayo imekuwa mwilini mwake na kufikia uzito wa takriban kilo ishirini.

Kudenya anasema anausikia uzito wa busha ukimlemea mwilini.

Ripoti: Aboubakar Famau