Uchaguzi Tanzania 2020: Mahona,Rungwe wataka raia kuhudhuria kampeni kuelewa sera za wagombea

Maelezo ya video, Uchaguzi Tanzania 2020: Mahona,Rungwe wataka raia kuhudhuria Kampeni
Iliyochapishwa

Wakati Kampeni za wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi za vyama mbalimbali zikiendelea nchini Tanzania, baadhi ya wagombea wamekuwa wakitoa vipaumbele ambavyo wamesema dhana zake zimekuwa 'zikitafsiriwa vibaya' na wananchi.

Hashim Rungwe,mgombea urais kwa tiketi ya chama cha CHAUMMA anaeleza dhana yake ya 'chakula' , hali kadhalika mgombea wa NRA Leopold Mahona.