Virusi vya corona: Catherine Wanjoya alivyobuni mashine ya kuteketeza barakoa zilizotumika

Maelezo ya video, Virusi vya corona: Catherine Wanjoya alivyobuni mashine ya kuteketeza barakoa zilizotumika
Iliyochapishwa

Katika kipindi hiki cha janga la Covid-19,usalama wa watu ni jambo la kipaumbele.

Vifaa vya PPE vinalenga kusaidia changamoto hii ya kiafya.

Lakini kwa upande mwingine, husababisha uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa. Na kutokana na hali hiyo basi ndipo ubunifu wa Catherine Wanjoya unapoingia.

Amebuni mashine maalumu ya kuteketeza vifaa vya kujikinga, PPE.

Mashine hizi ni muhimu sana kwenye vituo vya afya. kifaa hiki ni rahisi kukibeba na ni mahsusi kwa vituo vidogo vya afya.

Picha na Anne Okumu/ Judith Wambare.