Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Tanzania 2020: Kuna athari kwa wanamuziki kujihusisha na kampeni za kisiasa?
Uchaguzi mkuu nchini Tanzania utafanyika Oktoba 28 mwaka huu, huko Uganda, raia watawachagua madiwani, wabunge na Rais
Kwa kawaida katika nyakati hizi wasanii hutumika kuwavutia wanachama na wapenzi wa vyama mbalimbali ili kushiriki katika kampeni zao.
Nchini Tanzania, baadhi ya wasanii maarufu wamekua wakitunga nyimbo za kusifia chama ama viongozi wanaowaunga mkono.
Je, kuna athari za wao kufanya hivyo katika kuwaongeza au kuwapoteza mashabiki ambao hawana ufuasi wa chama chochote cha kisiasa?
Roncliffe Odit amewauliza maswali hayo John Kitime ambaye ni msanii nguli wa muziki kutoka Dar es Salaam Tanzania na Kidis The Jembe, mwanamuziki maarufu kutoka Nairobi Kenya.