Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke mwenye macho ya bluu afunga ndoa tena na mumewe baada ya kupatana
Risikat Azeez, mwanamke mwenye macho ya buluu kutoka Kwara na mume wake, Wasiu Omo-Dada, inaripotiwa kwamba wameoana tena.
Wawili hao hatimaye wametatua tofauti zao na kufunga pingu za maisha. Mwanamke huyo wa watoto wawili alikuwa amemshutumu mume wake kwa kuwatelekeza yeye na wanawe wawili kwasababu macho ya bluu.
Lakini muda mfupi baada ya taarifa yake kusambaa mtandaoni, mume wake ambaye walikuwa wametengana Omo Dada alijitokeza na kuanza kuzungumzia upande wake na hatimaye wakafikia maridhiano.
Awali, Mwanamke huyo alisema kwamba ameachana na mume wake. Yeye na watoto wake wanakabiliana na unyanyapaa kutoka kwa watu ambao walifikiri macho yao yaliwafanya kuwa wachawi. Aliisimulia BBC maisha yake...