Wanawake wataabika kupata dawa za uzazi wa mpango kwasababu ya corona
Iliyochapishwa
Wanawake milioni 47 kote duniani inasemekana kwamba watashindwa kupata dawa za kupanga uzazi ikiwa masharti ya Covid-19 yataendelea kwa miezi sita zaidi. Hiyo ni kulingana na Hazina ya Idadi ya Watu ya Umoja wa Mataifa. Lakini huko Kampala kuna ubunifu mmoja uliojitokeza kuhakikisha wanawake wanaendelea kupata huduma hiyo ya uzazi wa mpango ambao ni utumiaji wa boda boda.