Kim Jong-un ampatia dada yake Yo-jong 'majukumu zaidi'

Kim Yo Jong, dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, attends wreath laying ceremony at Ho Chi Minh Mausoleum in Hanoi, Vietnam March 2, 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kim Yo-jong dada yake Kim Jong-un
Iliyochapishwa

Rais wa Korea Kasakazini Kim Jong-un amempatia majukumu zaidi dada yake Kim Yo-jong, Shirika la ujjasusi la Korea Kusini limesema.

Bw. Kim bado amesalia "mamlaka kamili", lakini amepeana majukumu mengine hasa yanayohusiana na sera ili kujipunguzia mzigo wa kazi, shirika hilo la ujasusi limeripotiwa kusema .

Bi Kim sasa "anasimamia masuala yote kitaifa", Shirika la kitaifa la ujasusi limeongeza.

Hata hivyo, Shirika hilo la Seoul lishawahi kukosea kuhusu masuala ya Korea Kaskazini siku zilizopita.

Madai hayo yaliripotiwa kutolewa katika mazungumzo ya faragha siku ya Alhamisi katika bunge la taifa la Korea Kusini.

Wabunge baadae wakatoa tamko lao kuhusu suala hilo kwa wanahabari.

"Kim Jong-un bado amesalia na mamlaka yake kama kiongozi wa nchi, lakini amekuwa akipeana baadhi ya majukumu yake pole pole," shirika hilo limenukuliwa kusema.

Bi Kim sasa anasimamia sera za Pyongyang nchini Marekani na Korea Kusini, miongoni mwa masuala mengine ya, na ndiye "kiongozi mkuu wa pili," iliongeza, japo ilisisitiza kuwa Bw. Kim "hakumchagua mrithi wake."

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wametilia shaka madai hayo, huku tovuti ya NKnews ikisema kuwa alikosa mikutano miwili muhimu mwezi huu, hali ambayo inaongezea uzito madai ya waangalizi wa masuala ya nchi hiyo kwamba huenda ameshukishwa madaraka.

Kim Yo-jong ni nani?

North Korean leader Kim Jong Un and his sister Kim Yo Jong attend a meeting with South Korean President Moon Jae-in at the Peace House at the truce village of Panmunjom inside the demilitarized zone separating the two Koreas, South Korea, April 27, 2018

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kim Jong-un na Kim Yo-jong wanasemakana kuwa na uhusiano wa karibu sana

Akiaminiwa kuzaliwa mwaka 1987, ni mtoto wa kike wa mwisho wa hayati kiongozi Kim Jong-il na ni dada yake wa tumbo moja Kim Jong-un. Anazidiwa umri na kaka yake kwa miaka minne na inasemekana kwamba wana uhusiano wa karibu sana.

Anasemekana kuolewa na mwana wa Choe Ryong-hae, katibu wa chama tawala.

Bi Kim alianza kuangazia kimataifa mara ya kwanza mwaka 2018, alipokuwa mtu wa kwanza katika familia ya Kim kuzuru Korea Kusini. Alikuwa sehemu ya ujumbe wa olimpiki ya majira ya baridi, ambayo Kaskazini na Kusini zilishirika kama timu moja .

Pia alifanya kazi pamoja na ndugu yake katika makongamano ya kimataifa, ikiwemo kukutana na Marais wa Korea Kusini Moon Jae-in, Xi Jinping wa China na Rais wa Marekani Donald Trump.

Presentational grey line

Uchambuzi

Hapana shaka kwamba ushawishi wa Kim Yo-jong unaendelea kuongezeka.

Baadhi ya wachambuzi wanaamini mzozo wa mwanzo wa mwaka kati ya Kaskazini na Kusini uliochangia kulipuliwa kwa ofisi ya pamoja ya ushirika umempatia jukwa kubwa la kisiasa.

Alitoa taarifa hotuba yake ya kwanza kwa umma mwezi Machi. Lilikuwa tamko la kushambulia vikali Kusini. Baadae ilisem akuwa amepewa "idhini na kiongozi mkuu, chama chetu na taifa".

Pia aliandika waraka kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa mkutano kati ya Kim Jong-un na Rais Trump baadae mwaka huu, akisisitiza kuwa Korea Kaskazini haina " nia ya kuwa tishio kwa Marekani".

Hatua hizi zinaashiria kwamba huenda amepewa jukumu la kusimamia sera ya nchi hiyo kwa Marekani na Korea Kusini.

Presentational grey line

Shirika la ujasusi la Korea Kusini linaaminika kiasi gani?

Korea Kaskazini ni moja ya inayoendeshwa kwa usiri mkubwa duniani

Shirika la kitaifa la ujasusi la Korea Kusini huenda ina taarifa nyingi za kijasusi kuhusu Korea Kaskazini kuliko mashirika mengine, lakini inarekodi za kutatanisha.

Kwa mfano, mwaka 2016,vyombo vya habari vya Korea Kusini viliangazia taarifa kama hizi zilizotolewa na shirika la ujarusi zikisema kuwa mkuu wa majeshi ya Korea Kaskazini, Ri Yong-gil, alikuwa ameuawa.

Miezi mitatu baadae , serikali ya Korea Kusini ilisema kuwa yuko hai , baada ya jina lake kujumuishwa kati orodha ya maafisa wa chama.

Mwaka 2017, shirika hilo la ujasusi pia lilikiri kuwa lilijaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi wa wa urais wa mwaka 2012 upandeini.