Mzozo wa Libya: Kwanini Misri inaweza kutuma vikosi kumsaidia Jenerali Haftar?

Chanzo cha picha, AFP
Tafakari nyumba ya jirani inachomeka na hakuna wazima moto ambao unaweza kuwaita kuja kuzua janga ambalo linakaribia kukuathiri wewe na familia yako.
Hivyo ndivyo jinsi Msri imekua ikichukulia Libya tangu kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi na utawala wake mwaka 2011.
Libya haina taasisi za serikali zinazofanya kazi vizuri, hakuna jeshi la Umoja au vikosi vya usalama vya kutegemewa, na la msingi hakuna walinzi wa ndani na wa mpaka wa jangwani wenye urefu wa maili 1,100 (maili 685). Nchi hiyo pia ina watu wenye silaha haramu kila upande.
Mzozo uliibuka baada ya Walibya kushindwa kukubaliana juu ya njia ya kusonga mbele, wanamgambo wa kila aina wakaongezeka na makundi ya kijihadi yakajitokeza tena kutimiza ndoto zao za kuunda utawala wa Kiislamu nchini Libya na kwengineko.
- Misri ambayo - ilimuondoa madarakani Rais wa Kiislamu Mohammed Morsi 2013, na kumfunga pamoja na viongozi wengine wa kundi la Muslim Brotherhood - ilianza kushambuliwa:
- Juni 2014, majambazi waliwaua walinzi sita wa Misri mpakani
- Mwaka 2017, kundi la kijihadi lilivuka mpaka na kuingia katika himaya ya Misri na kuwashambulia maafisa wa usalama mpakani, ambapo askari 16 waliuawa na wengine 13 kujeruhiwa.
- Ndani ya Libya kwenyewe, wafanyakazi wa Misri walilengwa. Mwaka 2015 wanamgambo wa kundi la Kislamu la Islamic State waliwateka na kuwakata vichwa waumini 21 wa Kikristo kutoka
Misri, katika kile kilichodai kuwa hatua ya kulipiza kisasi kuondolewa madaraknai kwa Rais Morsi.
Hatua ya kuondolewa madarakani na kuaawa kwa Gaddafi Libya - kulisababisha mzozo mkubwa wa kisiasa karibu eneo zima la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
Hali imekuwa ya mvutano kati ya wale wanaoshinikiza siasa za kidini, zinazoendeshwa na kundi la Muslim Brotherhood na wale wasioegemea mfumo wa utawala wa kidini.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa uliopelekea kubuniwa kwa serikali ya mpito mjini Tripoli haukufanikiwa kufikia lengo la kupata maridhiano ya kitaifa ambayo ilikuwa msingi wa kuundwa kwake.
Muingilio wa Uturuki
Baada ya Libya kugawanyika kati ya Utawala wa Kiisalamu ulioungwa mkono na magharibi na ule unaopinga utawala huo unaoungwa mkono na Mashariki- Misri ambayo ilitangaza kundi la Muslim Brotherhood kuwa kindi la kigaidi moja kwa moja iliungana na mtu ambaye alitangaza vita dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Libya, Jenerali Khalifa Haftar.
Alikabiliana na makundi hayo na kuyaangamiza katika mji wa Benghazi na miji mingine mikuu ambayo ilikuwa inashikiliiwa na makundi hayo mashariki na kusini.

Chanzo cha picha, Reuters
Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, lengo kuu la Misri limekuwa kudhibiti hali katika mpaka wa Libya kwa kumpatia usaidizi Jenerali Haftar.
Lakini mambo yaligeuka katika eneo la Ghazal mwaka jana baada ya Uturuki - mshirika mkuu wa siasa za Kiislamu katika eneo hilo - kuamua kuunga mkono serikali ya mpito iliobuniwa chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa.
Ilitoa usaidizi wa kiufundi kwa serikali ili kukomesha hatua ya vikosi vya Jenerali Haftar kuteka mji wa Tripoli.
Baada ya kupata nguvu mpya kutoka kwa Uturuki Utawala wa Tripoli umeapa kukomboa maeneo yote nchini na kumshinda Jenerali Haftar.
Kumekuwa na ripoti kwamba Uturuki imewahamisha maelfu ya mamluki kutoka Syria na wapiganaji wa kijihadi mjini Tripoli na kuweka kambi yake kusini mwa Libya, sasa Cairo inadaiwa ilihisi ipo haja ya kujibu hatua hiyo.
Mwezi Juni, baada ya kuonekana akikagua zana za kivita akiandamana na wakuu wake wa ngazi ya juu jeshini katika kambi moja karibu na mpaka wa Libya, Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangazo la hatimaye kuingilia mzozo wa Libya.
'Msitari mwekundu'
Akiashiria Umoja wa nchi za Kiarabu, alisema, ikizingatiwa ushirikiano wa kihistoria kati ya watu wa Libya na Misri, Cairo ina haki ya kuingilia kati na kulinda maslahi ya kitaifa ya nchi hizo mbili dhidi ya "njama za kigeni".
Hakutaja Uturuki moja kwa moja, lakini kila maja alielewa mlengwa ni nani. Ujumbe wa Libya uliojumuisha viongozi wa kikabila ulimshangilia.

Rais Sisi aliwahi kuchora msitari mchangani - kati ya Sirte eneo la Mediterranean na maeneo Karibu na kambi ya jeshi ya Jufra kati ya Libya - na kuutaja kuwa "Mstari mwekundu" wa Misri.
Jaribio lolote la wanamgambo wanaounga mkono Tripoli kuvuka mstari huo litakuwa tisho kwa usalama wa kitaifa, alisema.
Siku chache baadaye, bunge la Misri liliidhinisha hatua ya Rais, ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa vikosi vyote vya usalama , kupeleka vikosi nchini Libya endapo kutakuwa na sababu ya kufanya hivyo.
Utawala wa Tripoli - ulighadhabishwa na tisho la Rais Sisi kuingilia Libya kijeshi, na kulitaja kama hatua ya "kutangaza vita".

Chanzo cha picha, Getty Images
Je! hili ni tisho la kweli ama uchokozi tu ?
Wachambuzi nje ya Misri wamekuwa wakihoji uwezo wa jeshi la Misri.
Lakini nchini humo mjadala wa umma kuhusu jeshi na utendakazi wake umepigwa marufuku.
Vyombo vya habari vimempongeza Rais na kusifu jeshi la nchi hiyo kama moja ya majeshi imara duniani, na hata kuilinganisha na majeshi ya Uturuki, na kudai kuwa ni chombo kinachotumiwa na Rais Recep Tayyip Erdogan na kuongeza kuwa Walibya "wanatumiwa" na utawala wa Tripoli.
Yasioweza kuepukika
Hatahivyo, baadhi ya watu walio na misimamo ya kadri wamekuwa wakihofia kwamba Misri huenda ikajipata katikati ya mzozo wa Libya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi la Misri lilihofia kuingilia kati mzozo huo, kwa sababu lingehitaji njia ya kupitisha silaha kati ya nchi hiyo na Libya - hali ambayo hatimaye ingelizua ugomvi.
Pia kulikuwa na hofu kwamba hatua ya Misri kuingilia kati mzozo huo ingelisababisha mgogoro kati ya vikosi vya majeshi na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu.
Waangalizi wanasema kuwa jeshi la Misri halijawahi kushiriki katika mapigano tangu 1973 lilipokabiliana na Israel katika mfereji wa Suez Canal na jangwa la Sinai.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makabiliano ya hivi karibuni ya jeshi hilo dhidi ya wanamgambo wa Kiislam kaskazni mwa Sinai hayakuwa ya kuridhisha.
Lakini baada ya kutoa onyo la kuingilia kati mzozo wa Libya, Misri sasa imejipata katika njia panda:
- Kuchukua hatua ya mapema kuvunja jaribio la kuteka miji ya Jufra and Sirte, hali ambayo itatibua mapigano ambayo inajaribu kuzuia.
- Ama kusubiri hadi upande wa pili kuvuka msitari iliyoweka, hatua ambayo huenda ikalemaza juhudi za Misri na washirika wake wa Libya.












