Enoch Adeboye: Mchungaji maarufu wa Nigeria aliyezua gumzo la ubaguzi wa kijinsia

Chanzo cha picha, PASTOR E. A. ADEBOYE
Enoch Adeboye, anayefahamika zaidi kama "Daddy Go" (Baba Msimamizi Mkuu), ni mchungaji wa Nigeria anayependwa na mamilioni ya wafuasi wake, lakini ambao pia wamekua wakimkosoa kwenye mitandao ya kijamii kwa kile wanachosema ni hurka yake ya ubaguzi wa kijinsia.
Mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 78- aliwekwa katika kiwango cha wachungaji wenye mapato ya chini miongoni mwa wachungaji matajiri wanaotoa mahubiri kwa njia ya televisheni katika taifa hilo lililoko magharibi mwa Afrika, lakini amekua maarufu sana.
Amekuwa mkuu wa kanisa linalofahamika kama Redeemed Christian Church of God (RCCG) kwa karibu 40 - na chini ya uongozi wake thabiti kanisa hilo limekuwa kwa kiwango kikubwa.
Ni nadra kuupata mtaa wa eneo la kusini mwa Nigeria linalokaliwa na Wakristo wengi bila kanisa la RCCG, baadhi ya mitaa hata huwa na makanisa mawili-na nembo yake ya njiwa imekuwa ni sehemu ya utambulisho wake.
Lakini maoni ya mchungaji juu ya ndoa na majukumu ya kijinsia yamekuwa yakiwashangaza baadhi ya watu katika enzi hii ya age kampeni ya #metoo - hata katika taifa hili lenye itikadi.
''Oa mwanamke anayeweza kupika''
Amekuwa mtoa maoni wa mara kwa mara katika mitandao ya kijamii kwa kipindi cha muongo uliopita-na wakati alipotuma baadhi ya "masomo " kwa ajili ya wanawake katika siku ya kuzaliwa ya mke wake mwezi Julai, yalipoingia kwenye mtandao wa Twitter yaliibua mjadala mkubwa juu ya haki za wanawake na usawa wa jinsia kati ya mwanamke na mwanaume.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Hata kama umesoma vipi au una mafanikio kiasi gani , mume wako ni kichwa chako na unapaswa kumuona hivyo wakati wote'' alitweet kwa wafuasi wake milioni 1.3.
Kwenye Instagram aliongeza kumuhusu mke wake : "Haijalishi ni nini amepanga juu ya safari yake, kama nikisema ningependa uende na mimi mahali fulani na mahali fulani…lazima ataahirisha chochote alichotaka kukifanya na kusafiri na mimi''
Katika ujumbe alioutuma mwezi Januari , alimshauri mtoto wake wa kiume ambaye ameoa kumfuta kazi katibu wake "anayetarajia kumuona kazini ", jambo ambalo halikufurahiwa .
Na mwaka 2016 alikua na ushauri huu kwa ambao hawajaoa : "Usioe msichana ambaye ni mvivu . Usimuoe msichana ambaye hawezi kupika. Anahitaji kufahamu jinsi ya kutekeleza majukumu yake na kupika kwasababu huwezi kuwa unakula nje wakati wote."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe

Hotuba zake kupitia televisheni kwa zinawakera wanaharakati wanawake lakini si wote wanaoyapokea kwa mtizamo hasi, ukweli unaodhihirishwa na mafanikio ya kanisa lake, ambalo analiendesha kama biashara.
'Misaada ili ufike mbinguni'
Kila Jumapili, kabla kupigwa marufuku kwa mikusanyiko mikubwa ya watu kwasababu ya virusi vya corona, maelfu ya watu waliingia katika milango ya kanisa la RCCG kote duniani, wakitafuta miujiza, kuokolewa, maisha ya milele au kutatuliwa matatizo ya kifedha.

"Ninataka kuwa upande wa Mungu, kulindwa na imani ya kikristo, nilipata hili katika RCCG. Binafsi , ninataka kwenda mbinguni ," alisema mmoja wa wafuasi wa kanisa hilo katika mji mkuu Abuja, ambako kuna uwanja mkubwa wa maombi viungani mwa mji mkuu.
Wengine wanasema walivutiwa na Mchungaji ''utakatifu''na ''unyeyekevu'' pamoja na "kutekeleza anayoyafundisha".
Wale wanaoingioa kanisani wanafurahia kutoa misaada au kununua bidhaa za kumbukumbu.
Wengi wao wanakukbali kutoa 10% ya mapato yao kwa kanisa, kama fungu la kumi.
"Yeyote ambaye halipi fungu la kumi haendi mbinguni, hiyo ndio ukweli ," aliwaambia wafuasi wake miaka miwili iliyopita.
Ni vigumu kufahamu kiwango cha utajiri cha Mchungaji Adeboye, kwani ni vigumu kutambua ni kiasi gani cha mali ya kanisa na mali yake binafsi inayokadiriwa kuwa kati ya dola milioni 60 (£46m) na milioni 130.

Chanzo cha picha, RCCG
Hii inamuweka profesa huyo wa zamani wa hesabu katika Chuo kikuu cha Lagos , ambaye amekataa kuongea na vyombo vya habari katika ligi moja na nyota wa muziki nchini humo na tajiri zaidi kuliko wachezaji wengi wa kulipwa wa Nigeria wanaocheza soka la kulilpwa katika mataifa ya kigeni.
Lakini kando na tai yake ndogo shingoni na suti yake ya safari na shati yenye mistari, haonekani nadhifu ukilinganisha na viwango vya wachungaji wenzake wa makanisa ya Kipentekoste ambao huvaa mavazi ya kung'ara na nadhifu zaidi.
Hana viatu vya kung'ara, hana nywele zilizopakwa mafuta mengi, Kiingereza chake hakipandi na kushuka kwa lafudhi ya Kimarekani.
Alizaliwa katika familia masikini, ni mtu mnyeneykevu, na wale walio karibu nae humuelezea hivyo zaidi.
Lakini, yeye au -kanisa lake wanamiliki Chuo Kikuu ,ndege aina ya Jet - Gulfstream jet na magari kadhaa ya kifahari.
Haegamii upande wowote katika siasa
Mchungaji r Adeboye pia ana nguvu kisiasa-na anaheshimiwa vizuri na Wanaigeia wenye kipato cha kati wanaoishi maeneo ya miji ya Nigeria.

Mchungaji Enoch Adejare Adeboye
- 1942: Alizaliwa katika eneo la Ifewara, jimbo la Osun , kusini-magharibi mwa Nigeria
- 1967: Alipata shahada yake ya kwanza ya hisabati
- 1967: Alimuoa Foluke Adeyokunnu
- 1977: Alitawazwa kuwa mchungaji wa kanisa la RCCG
- 1981: Alikuwa msimamizi mkuu wa kanisa la RCCG

Katika kampeni za uchaguzi wa rais, baadhi ya wagombea walitekeleza jukumu lao la kutembelea kanisa lake kwa maombi ili waonekane wakiomba na kusalimiana nae-na picha zake za wavuti zinamuonesha akiwasalimia viongozi wa dunia.
Maoni yake kuwahusu wanawake -ambapo mara kwa mara huwa anayatoa kwenye biblia-yanaonekana na baadhi ya watu kama jambo lisilo la kushangaza, hata kama baadhi wanasema aya hizo za biblia zinaweza kufafanuliwa kwa njia nyingine. ways.
"Ukristo na dini huimarisha mfumo dume , kwa hiyo sio jambo la kushangaza kuwa viongozi wa kidini wankuwa na mtazamo wa aina hiyo ," anasema Martha Edem,mwandishi wa vitabu vya kikristo.
Alielezea "tweet za Mchungaji za siku ya kuzaliwa " kama fursa iliyopotea ya kuwafundisha wanandoa kuheshimiana na upendo. Lakini hata baadhi ya wanaharakati wa jinsia katika nchi zilizoshika dini hawataki kumpinga
"Kwangu mini inatokana na vile ambavyo mtu anaelewa…Siwezi kumuhukumu mtu wa Mungu, Ukristo ni dini ya imani ," mwanaharakati wa jinsia na msomi Abigail Ogwezzy-Ndisika alisema.
Utajiri wa wachungaji wakubwa wa Nigeria mara nyingi huwafanya kuwa walengwa mara kwa mara wa wale wanaowaona kuwa wanawatumia watu vijbaya kujitajirisha
Baadhi wanasema Mchungaji Adeboye anapaswa kutumia ushawishi wake zaidi kwa wanasiasa-kwasababu hata Makamu wa rais wa sasa Yemi Osinbajo ni Mchungaji katika kanisa la RCCG.
Kusema ukweli, aliendesha maandamano ya amani mweiz Februari kuzungumzia suala la usalama mbaya nchini.
Ameonyesha kuwa anatambua kuwa anachunguzwa uhusiaka wake katika siasa- haegemei chama kimoja wala kingine.
Lakini wale wanaomtarajia awe mtu asiyeegamia zaidi upande mmoja katika ndoa itawabidi wasubiri kwa muda mrefu.












