Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mlipuko Beirut: ‘Ghafla nilipoteza uwezo wa kusikia’
Iliyochapishwa
Utafutaji wa walionusurika mlipuko mkubwa wa Beirut unaendelea nchini Lebanon ambapo watu wasiopungua 300 walipoteza maisha huku maelfu ya wengine wakijeruhiwa.
Walioshuhudia wameelezea tukio hilo la kuogofya ikiwemo mwanahabari wa BBC Arabic Maryem Taoumi, aliyerushwa na nguvu ya mlipuko wakati anafanya mahojiano.
Rais wa Lebanon Michel Aoun anasema tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate zilikuwa zimehifadhiwa kwa njia isio salama katika ghala moja na kusababisha mlipuko.