Virusi vya corona: Mchimbaji makaburi Somalia ahusisha idadi kubwa ya watu wanaokufa na maradhi hayo

Maelezo ya video, ‘Mchimbaji makaburi‘ Somalia aelezea hali inayotia hofu
Iliyochapishwa

Nchini Somalia, madaktari vijana wawili wanapigania maisha yao. Wakati ambapo ugonjwa wa virusi vya corona umesababisha kifo kwa mwathirika wa kwanza, wamejitolea katika hospitali moja tu iliyotengwa kwa wagonjwa wa virusi vya corona. Lakini licha ya ujasiri wao, watu wanakufa kwasababu hospitali hiyo haina vifaa muhimu vya matibabu.

Idadi rasmi iliyotolewa ni kwamba raia wa Somalia waliokufa na Covid-19 ni chini ya 100. Lakini BBC Africa Eye imetembelea moja ya eneo kubwa la makaburi ambapo wachimbaji makaburi wanaelezea hali tofauti.