Wamarekani wanaoamini Trump anaunusuru ulimwengu na kundi la walawiti

Iliyochapishwa

Nchini Marekani kuna nadharia ya ajabu ambayo imekuwa maarufu miongoni mwa watu nchini Marekani tangu janga la corona lilipoikumba Marekani. Wanaofuata nadharia hiyo wanaamini kuwa rais wa Marekani Donald Trump yuko mamlakani kuinusuru dunia dhidi ya makundi ya kishetani ya walawiti wa watoto. Ni ni vipi nadharia hii limewavutia watu wengi? BBC imezungumza na ndugu na waumini wa nadharia hiyo kubaini zaidi.