Virusi vya corona: Wasichana wanaotengeneza mashine zinazowasaidia wagonjwa wa corona kupumua

Maelezo ya video, Wasichana wa Afghanstan wanaotengeneza mashine za kupambana na corona
Iliyochapishwa

Timu ya wasichana pekee kutoka nchini Afghanstan imeelekeza juhudi zake katika kuwasaidia wagonjwa wa Covid-19- kwa kutengeneza mashine za bei nafuu (ventilator). Wasichana hao wenye umri wa kati ya miaka 14 na 17, wanatumaini kuwa ubunifu wao utatumiwa katika hospitali na watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa mashine hizo katika nchi yao ambayo imeagiza chache kutoka nje.