Virusi vya corona: Vikosi vya usalama Uganda huenda vikawa hatari zaidi kuliko virusi vya corona

Joyce Namugalu Mutasiga pressing out pancakes from pastry
Maelezo ya picha, Eric Mutasiga's mother, Joyce Namugalu Mutasiga, has to support his family after he was killed by police
Iliyochapishwa

Nchini Uganda, watu wasiopungua chini ya 12 inasemekana kwamba wameuawa na maafisa wa polisi wanaotekeleza hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi corona huku kukiwa hakuna hata mtu mmoja ambaye amekufa kwa sababu ya virusi vya corona vyenyewe. Patience Atuhaire mwanahabari wa BBC amekuwa akikutana na baadhi ya walioathirika na matukio hayo.

Joyce Namugalu Mutasiga amezungumza nae wakati anapika chakula cha Kiganda mfano wa chapati za maji kwa jina kabalagala, kwa kutumia jiko la kuni, maneno yake yakiwa yanakata kata.

"Mtu anaokuondokea ulipo kisha unampiga risasi? Basi wangeomba hata msamaha tu, kwasababu uhai wake hauwezi kurejea tena, sasa nitalazimika kuhangaika na watoto," anasema, huku akiwa na hisia.

Mama wa miaka 65, sasa ndio mtegemezi mkuu wa familia ya watoto wanane.

Joyce Namugalu Mutasiga making pancakes
Maelezo ya picha, Mrs Mutasiga wants the police to apologise over the death of her son

Wajukuu wake wawili, wakiwa na miaka mitatu na mitano, ni wadogo sana kubaini kilichotokea, wanakimbia huku na kule na kuonyesha gari lililo nyuma ya ua: "Wanapiga picha ya gari la baba wa familia!"

Juni, karibu wiki tatu baada ya kusemekana kwamba amepigwa risasi mguuni na polisi wa Uganda, Eric Mutasiga alikufa kwa jeraha alilopata. Dakika zake za mwisho alikuwa kwenye chumba cha kufanyiwa oparesheni hospitali kuu nchini humo ya Mulago, kulingana na mama yake.

Mwalimu mkuu aliyekuwa na umri wa miaka 30, ni miongoni mwa waliouliwa na vikosi vya polisi wakati wanatekeleza hatua za kutotoka nje kwasababu ya virusi vya corona.

Maafisa wa usalama katika barabara za mji

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa vikosi vya usalama waliotumiwa kuhakikisha amri ya kutotoka nje inazingatiwa

Inaaminika kwamba mauaji yanafanyika mikononi mwa polisi, wanajeshi na kikosi cha ulinzi wa raia kinachofahamika kama LDU.

Tangu Machi, kumekuwa na vizuizi barabarani kuhakikisha kwamba raia wanatekeleza kanuni zilizowekwa ikiwemo marufuku ya pikipiki na kutotoka nje usiku hadi asubuhi.

Raia wengi wa Uganda wana wasiwasi wakati wanakaribia kwenye maeneo ya ukaguzi barabarani kwasababu hawajui nini kitakachotokea, lakini Mei 13, kuna ghasia zilizotokea katika nyumba ya Mutasiga.

Baba huyo anayeendesha shule ya msingi ya Merrytime, baba wa watoto watatu alikuwa na duka dogo karibu na nyumba yake ikiwa ni mwendo wa saa moja kutoka mji mkuu wa Kampala.

Jumatano hiyo, maafisa wa polisi na kikosi cha LDU walikuwa wanakamata watu wanaovunja sheria ya kutotoka nje kwa kufanyakazi kazi baada ya saa moja usiku muda wa ukomo kutoka nje uliowekwa na serikali.

'Hamukunifunza'

Bwana Mutasiga mwajiriwa, kijana anayefanyakazi katika kibanda kimoja cha kuuza chapati nje ya duka, alikuwa tu ndio amekamatwa.

"Niliomba msamaha. Maafisa wawili wakawa wanajadiliana ikiwa watamuachilia aende," mwalimu huyo mkuu baadae alizungumza na mwanahabari wa eneo.

Lakini watu walipokusanyika mambo yakazidi kupamba moto.

A man's head with a scar
Maelezo ya picha, Mwanamume aliyejeruhiwa kichwani baada ya kushambuliwa

"Polisi mmoja akaanza kusema sio mimi niliyemfunza. Akasema kuwa anaweza hata kunipiga risasi.

"Wakati ninageuka kuondoka polisi mmoja akapiga risasi juu ya hewa. Nikageuka kuangalia kinachoendelea na nikamuona moja kwa moja amenilenga.

"Risasi ikanipiga mguu wangu wa kushoto na nikaanguka. Kwa haraka wakapanda kwenye pikipiki yao na kuondoka."

Alisema maneno hayo wakati anakimbizwa hospitali.

Baadhi ya wanafamilia wamependekeza twende mahakani lakini polisi haijasema ni polisi yupi aliyempiga risasi, sasa nitamushtaki nani?"

Transparent line

Familia ilikuwa na matumaini kuwa atapona.

"Tulikuwa hospitali kwa muda tunasubiri afanyiwe upasuaji lakini kila tulipowauliza wahudumu wa afya walituambia kwamba kidonda hicho kiko vibaya sana hawangeweza kumfanyia upasuaji," mama yake anasema.

Bwana Mutasiga hatiame akapelekwa kwenye chumba cha upasuaji Juni 8 ambapo aliaga dunia, ameongeza.

Cheti cha kufa kinaonesha kwamba alikufa kwa jeraha la bunduki.

Mke wa Mutasiga anaangalia chini na kuchukua muda kidogo kujipa moyo kabla ya kuzungumza.

Anahisi kuwa mfumo mzima wa serikali umeshindwa kutekeleza jukumu lake: "Baadhi ya wanafamilia wamependekeza twende mahakani lakini polisi haijasema ni polisi yupi aliyempiga risasi, sasa nitamushtaki nani?"

Short presentational grey line

Farida Nanyonjo amekasirika.

Kaka yake, Robert Senyonga, alikufa baada ya kupigwa.

Karibia mchana Julai 7, akapokea simu kutoka kwa mwajiri wake. Akaambiwa kwamba anahitajika mashariki mwa mji eneo la Jinja haraka kwasababu Bwana Senyonga amepigwa mara kadhaa kwa kitako cha bunduki na mtu anayeaminika ni kutoka kikosi cha LDU kwasababu ya kuendesha pikipiki.

Presentational grey line

Pia unaweza kusoma:

Presentational grey line

Kichapo alichopata kilimuacha kijana huyo, 20, aliyekuwa anafanyakazi kama msimamizi wa shamba na majeraha baada ya fuvu lake la kichwa kupasuka.

Bi. Nanyonjo alimpata usiku na kurejea nae mjini, ambapo aliagizwa kwenda hospitali.

"Tulifika hospitali kuu ya Mulago karibu saa nane usiku, na kumaliza usiku huo tukiwa tumelala kwenye ushoroba. Nilimfuata mhudumu mmoja anisaidie lakini akaitisha pesa. Na hatiame akapewa kitanda asubuhi," anasema.

Ilichukua siku kadhaa kabla ya Bwana Senyonga kupangiwa kufanyiwa upasuaji. Lakini ulikuwa umechelewa sana.

'Alikufa mikononi mwangu'

"Ninahasira sana. Walimpiga lakini hata hospitali kubwa nchini haikuweza kumpa matibabu bora," Bi. Nanyonjo anase,a

"Kaka yangu alikufa mikononi mwangu."

Kwa familia hii, pengo lililoachwa na mwendazake hakuna mtu anaweza kulijaza.

Kikosi cha LDU kilianza kuwa na sifa mbaya miaka ya 2000s lilipoanza kuundwa. Maafisa wake walikuwa wanashtumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kiholela au kubadilika na kuwa watu wenye silaha wanaoweza kukodishwa.

Mwishoni kikosi hicho kikavinjwa. Lakini raia walikuwa na wasiwasi baada ya kufahamu kwamba kikosi hicho kimefufuliwa tena 2018.

Wnaume akifanya mazoezi

Chanzo cha picha, Allan Atulinda

Maelezo ya picha, Shughuli ya kuwasajili maafisa wapya wa ulinzi iliwavutia vijana wengi 2018

Wakosoaji wanasema kikosi hicho kinatoa silaha kwa vijana wadogo ambao hawajapewa mafunzo ya kutosha wasioweza kupunguza uhasama na wasiwasi wakati wa makabiliano.

Jeshi sasa hivi limeondoa maafisa wote wa LDU waliokuwa wametumwa kuhakikisha sheria inafuatwa katika maeneo mbalimbali ili kupewa tena mafunzo.

Rais Yoweri Museveni na maafisa wengine waandamizi wameshutumu mashambulio ambayo yameripotiwa lakini BBC ilipowasiliana na mashirika kadhaa ya usalama, hakuna lililotoka kutoa taarifa yao kuhusiana na madai hayo.

Makundi ya haki za binadamu yanasema kwamba hilo ni tatizo la kimfumo.

"Tumebaini kwamba vikosi vya usalama vimekuwa vikitumia ugonjwa wa Covid-19 na hatua zilizowekwa kuzuia usambaaji wake kama kisingizio cha kukiuka haki za binadamu," amesema Oryem Nyeko, mtafiti wa shirika la Human Rights Watch.

Lakini matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, anasema, na "kuna haja ya kufanya mabadiliko kwenye mfumo unaohamasisha watu kutekeleza unyanyasaji".

Familia zinasema kuwa mfumo wa mahakama mara nyingi huwa unakanganya lakini kumekuwepo na visa viwili ambapo washtakiwa wamepatikana na hatia katika kipindi cha miezi mitano iliyopita. Moja ikiwa ni ya mwanajeshi na nyengine ya afisa wa LDU

Coronavirus in Uganda. Total number of cases. Total number of coronvirus cases in Uganda Figures were recalculated on 21 May.
Transparent line

Benon Nsimenta, aliyekuwa anasubiri kutawazwa kama reverendi Novemba, alipigwa risasi kwenye barabara kuu magharibi mwa mji wa Kasese Juni, 24.

Yeye na mke wake walikuwa wametika kijijini kwa kutumia pikipiki na pia walikuwa na barua kutoka kwa mamlaka ya eneo inayoonesha usafiri ni wao.

"Wanajeshi waliotusimamisha hawakuchukua hata dakika moja kutuuliza chochote. Mmoja wao alivuka barabara akainua bunduki yake na kumpiga risasi mume wangu kwenye shingo," Bi. Musiimenta amesema.

"Tulikuwa tunafanya miradi ya familia pamoja, tunajadiliana kwa kila jambo. Tulizungumza kuhusu hatma ya watoto wetu. Nitalipia vipi ada yao ya shule kwa kufanyakazi tu kwenye shamba dogo?" anasema.

Short presentational grey line