Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi wagundua cocaine ikiwa imefichwa ndani ya maganda ya kahawa
Iliyochapishwa
Polisi wa Italia wamegundua dawa za kulevya aina ya cocaine zilizofichwa kwenye maganda ya kahawa, mzigo wa mtu mmoja ulitumwa kutoka Colombia.
Polisi wa uwanja wa ndege wa Milan Malpensa wamesema waliutilia shaka mzigo huo uliokuwa umetumwa kwa Santino D'Antonio, jina la kiongozi wa uhalifu katika filamu iitwayo John Wick: Sehemu ya pili.
Mwanaume huyo alikamatwa baada ya kujaribu kuchukua mzigo huo kutoka kwenye duka la tumbaku.