Pamoja na kupatikana haki ya wanawake kuendesha magari bado watetezi wanashikiliwa

Maelezo ya video, Pamoja na kupatikana haki ya wanawake kuendesha magari bado watetezi wanashikiliwa
Iliyochapishwa

Wakati mamlaka za Saudi Arabia chini ya uongozi wa Mwanamfalme Mohammad bin Salman ziliporuhusu wanawake kuendesha magari mwaka 2018, hatua hiyo ilisifiwa na wengi kuwa hatua uhimu katika kupatikana kwa uhuru zaidi katika nchi ambayo ilikuwa haikubali mabadiliko.

Lakini wanawake waliofungwa kutokana na kampeni ya kugombea haki ya kuendesha magari wameendelea kushikiliwa gerezani huku familia zao zikidai kuwa wanawake hao wamekuwa wakiteswa na kudhalilishwa kijinsia.