Mwanate Issa Rashid na safari yake ya ufundi mekaniki
Iliyochapishwa
Siku za hivi karibuni wanawake wengi wamekua wakijihusisha katika shughuli ambazo zimekua zinafanywana na wanaume kwa muda mrefu, lakini hivi sasa baadhi ya wanawake wameamua kujihusisha katika shughuli hizo ili kujipatia kipato na kuendesha maisha.
Mwanate Issa Rashid kutoka Mkoani Lindi amejitosa katika shughuli ya ufundi mekaniki, na wakati amenza anasema kuwa wanaume waliokua wakileta magari na vifaa vingine vya moto kutengenezwa hawakuamini juu ya ufanyaji kazi wake, kwakua ni mwanamke.
Lakini ana malengo gani na kazi yake hii?