Uchaguzi Tanzania 2020: Zitto aeleza makosa yaliyofanywa na muungano wa UKAWA katika uchaguzi uliopita

Iliyochapishwa

Wakati joto la uchaguzi nchini Tanzania likiendelea kupanda, Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani ACT-Wazalendo, chama kinachoendelea kukua kwa kasi, amezungumza na BBC juu ya masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi.

Bwana Kabwe amemweleza mwandishi wetu Sammy Awami kile anachoamini kuwa makosa yaliyofanywa na muungano wa vyama vya siasa uliojulikana kama UKAWA katika uchaguzi mkuu uliopita.

Amezungumzia pia kujiunga kwa mwanachama na mwanasiasa maarufu Bernard Membe na matumaini ya muungano wa vyama vya siasa katika uchaguzi ujao mwezi Oktoba.

Fuatilia mahojiano haya maalum, kusikia kwanini Kabwe anaamini muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu hauepukiki.