Virusi vya corona: Jinsi densi ya zumba inavyowasaidia wafanyakazi hawa walio mstari wa mbele kukabiliana na mlipuko huo

Maelezo ya video, Virusi vya corona: Jinsi densi ya Zumba inavyowasaidia wahudumu walio msatari wa mbele nchini Kenya
Iliyochapishwa

Kazi inayotumia muda mrefu, kukaa mbali na kujitenga na watu kunasababisha athari za kiakili miongoni mwa wahudumu wa afya , walio mstari wa mbele wakati huu wa janga la virusi vya corona. Kwahivyo katika hospitali hii ya magonjwa ya akili mjini Nairobi, Kenya wanajaribu kufanya kitu tofauti ili kuwasaidia kupumzisha akili na kuwatia moyo kuendelea na kazi.