Anthony Mmesoma Madu, mcheza densi wa miaka 11 aliyevutia mioyo ya watu mtandaoni

Iliyochapishwa

Video ya Anthony Mmesoma Madu mwenye umri wa miaka 11 iliyosambaa mitandaoni iliomuonyesha akicheza densi ya ballet kwenye mvua.

Video hiyo imesambazwa mitandaoni na nyota wa Hollyhood Viola Davis na wasanii wengine. Anthony ni miongoni mwa wanafunzi 12 wa shule ya Leap of Dance Academy jiji Lagos, Nigeria.

Shule ya Leap of Dance Academy ilianzishwa mwaka 2015 na Daniel Ajala Owoseni na amekuwa akiyatoa mafunzo ya ballet bila malipo kwa wanafunzi wake.