Tazama binti alivyovuruga mahojiano ya mama yake ya moja kwa moja kwenye Televisheni

Maelezo ya video, Binti mdogo aliyevuruga mahojiano ya mama yake na BBC News
Iliyochapishwa

Dkt Clare Wenham alikuwa anafanya mahojiano ya moja kwa moja na BBC News kuhusu hatua ya kutotoka nje Uingereza wakati ambapo binti yake mdogo alipojitokeza ghafla kwenye chumba alichokuwa anakitumia kuhojiwa.

Akizungumza na BBC baadae, Dkt Wenham alisema imekuwa kama kinaya hili kumtokea kwasababu alikuwa ameandika makala kwa Jarida la Kitabibu Uingereza kuhusu mada hiyo. Lakini asichokuwa anakifahamu wakati huo ni kwamba kile alichokiandika kingemtokea mwenyewe.