Wakulima wa ufuta wamelazimika kuuza ufuta karibu kwa nusu ya bei waliouza msimu uliopita
Iliyochapishwa
Shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida nchini Tanzania. Lakini kwa biashara ya mazao ya kilimo ambayo inategemea mazao ya nje, yenyewe bado inachechemea.
Na hii ni zaidi kwa mazao kama ufuta vile, ambao unalimwa zaidi Kusini mwa Tanzania.
Kutokana na kufungwa mipaka na masoko ya kimataifa, wakulima wa ufuta kusini mwa Tanzania sasa wanalazimika kuuza kilo moja ya ufuta kwa kama Dola senti 56 tu - takribani nusu ya bei waliyoiuza msimu uliopita ambayo ilikuwa zaidi ya Dola moja.
Mwandishi wetu Sammy Awami alikwenda Lindi, Kusini mwa Tanzania kujionea hali ilivyo.