Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Bernard Membe aeleza tofauti ya 'CCM ya zamani na CCM mpya'
Hapo Jana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na kada wa muda mrefu wa chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bernard Membe alirudisha kadi yake ya uanachama wa CCM kitendo kilichomaanisha ukomo rasmi wa uanachama wake CCM.
Wiki iliyopita alipozungumza na mwandishi wa BBC Sammy Awami, Membe alisema alikuwa bado ana imani ya kusafishwa na Halmashauri Kuu ya CCM na kurudishwa tena katika chama hicho baada ya kufukuzwa uanachama miezi michache iliyopita.
Katika mazungumzo hayo na BBC, Membe alielezea utofauti wa aliyoiita 'CCM ya zamani' na 'CCM mpya'. Hii hapa ndio sehemu ya mazungumzo hayo.